Home Podcasts Wanangu podcast
Wanangu podcast

Wanangu podcast

Goodluck Joseph 94 Episodes Sep 7, 2026

This podcast is hosted by Goodluck Joseph, a curious guy who likes to share all the things he finds interesting in the form of a podcast episode. In other words, this podcast is an extension of his personality and more. Expect to hear topics that range from music, movies, and books to random ideas, all presented in a creative manner.

Episodes

Episode 108 | Fikra Sahihi Huja Kwa Lugha Asili
Episode 108 | Fikra Sahihi Huja Kwa Lugha Asili Sep 7, 2026 810 Fuatilia jinsi mstari mmoja wa Nash Mc unavyoweza kuzalisha maswali mengi na yenye kutafakarisha kuhusu uhusiano na kutegemeana kati ya lugha na fikra. Ni kama hadithi ya nani alianza kati ya yai na kuku, lakini safari hii ikiwa katika uwanja wa lugha na utambuzi. Je, lugha ndiyo huchochea namna tunavyofikiri, au fikra ndizo huunda lugha tunayotumia?
Episode 107 | A.k.a Mimi by Ngwair (Uchambuzi)
Episode 107 | A.k.a Mimi by Ngwair (Uchambuzi) Aug 31, 2026 1538 Katika episode hii, Host anaichambua album ya kwanza ya Ngwair, A.K.A Mimi, na kueleza mambo aliyogundua baada ya kuisikiliza tena akiwa mtu mzima. Wakati album hii ilipotoka, alikuwa bado mdogo na huenda hakuwa na uwezo wa kuielewa kwa kina kama anavyoweza leo. Safari hii, anaisikiliza kwa mtazamo tofauti; akiunganisha “dots” zilizopo baina ya nyimbo, mambo yanayofanya album hii isimame kama kazi
Episode 106 | Usiamini Hadithi Moja Tu
Episode 106 | Usiamini Hadithi Moja Tu Aug 24, 2026 713 Katika episode hii, tunaangazia tabia ya kuchukua hadithi ya mtu mmoja na kuitumia kama ushahidi wa kuhitimisha jambo kubwa zaidi. Kupitia mifano ya maisha ya kila siku, katika afya, biashara na social media, tunaona jinsi kauli kama “Mimi ninamjua mtu ambaye…” zinavyoweza kutufanya tufanye maamuzi yasiyo sahihi. Episode hii inatukumbusha kwamba stori moja inaweza kuwa ya kweli, lakini isiwe ushah
Episode 105 | Kampuni Inayouza Rangi Bila Kuuza Rangi!
Episode 105 | Kampuni Inayouza Rangi Bila Kuuza Rangi! Aug 17, 2026 660 Katika Episode hii, tunaangazia historia ya kuvutia ya Pantone, mfumo uliobadilisha namna dunia inavyotambua, kuwasiliana na kutumia rangi. Tutafuatilia jinsi wazo la kuunda mfumo wa kutambua rangi lilivyoanza, namna Pantone ilivyogeuka kutoka kwenye mfumo wa kawaida wa kuchanganua rangi na kuwa sehemu muhimu ya ulimwengu wa ubunifu, mitindo, matangazo na biashara. Karibu!
Filamu ya Afrika Iliyowahamasisha Jay-Z na Beyoncé
Filamu ya Afrika Iliyowahamasisha Jay-Z na Beyoncé Aug 10, 2026 1277 Je, ni nini kinachofanya filamu iliyotengenezwa Afrika zaidi ya miaka 50 iliyopita iendelee kuzungumziwa, kupongezwa na hata kuwavutia mastaa kama Jay-Z na Beyoncé? Katika episode hii, host anasimulia Touki Bouki, mojawapo ya filamu kubwa na zenye ushawishi kuwahi kutokea Afrika. Tunafuatilia safari ya wahusika Mory na Anta, lakini zaidi ya hapo, tunaangalia kile ambacho filamu hii inakisema kuhus
Kupenda Kwangu 'Titles' Kunanigharimu
Kupenda Kwangu 'Titles' Kunanigharimu Jul 27, 2026 774 Katika episode hii, host anakukaribisha ndani ya mawazo yake na kukuonyesha mchakato halisi anaoupitia kila anapotafuta title ya episode mpya. Ni safari iliyojaa vita ya ndani kati ya kuandika title inayomridhisha yeye kama ‘mbunifu’ na ile inayopewa kipaumbele na mtandao (algorithms) ili kuwafikia watu wengi zaidi. Anaeleza mapenzi yake ya muda mrefu juu ya titles nzuri tangu akiwa mtoto, hadi ch
Episode 101 | Timamu Kati ya Wasio Timamu
Episode 101 | Timamu Kati ya Wasio Timamu Jul 20, 2026 1019 Katika episode hii, host anachambua utafiti maarufu uliofanywa na Dkt. David Rosenhan mwaka 1973, uliouliza swali muhimu kuhusu uwezo wa wataalamu wa afya ya akili kutofautisha kati ya mtu mwenye ugonjwa wa akili na anayejifanya kuwa nao. Matokeo ya utafiti huo yaliibua mjadala mkubwa na kuonyesha mapungufu yaliyokuwepo katika mfumo wa utambuzi wa magonjwa ya akili, kiasi cha kuwafanya wengi kuhoj
Episode 100 | Kwanini Iliitwa Wanangu Podcast?
Episode 100 | Kwanini Iliitwa Wanangu Podcast? Jul 13, 2026 1204 Host anaadhimisha kwa furaha kufikiwa kwa episode ya 100 ya Wanangu Podcast, akitoa shukrani za dhati kwa kila aliyekuwa sehemu ya safari hii, kuanzia wasikilizaji / watazamaji hadi marafiki waliotoa mawazo, ushauri na mchango wao katika kuiboresha podcast hii. Katika mazungumzo hayo, anasimulia pia chanzo cha jina Wanangu Podcast, sababu zilizomfanya alichague, na anagusia mafunzo makubwa aliyoji
Episode 99 | Tofauti Kati ya Single, EP na Album
Episode 99 | Tofauti Kati ya Single, EP na Album Jul 6, 2026 1117 Muziki hutolewa kwa mifumo tofauti kama Single, EP, na Album, lakini je, unafahamu tofauti kati ya aina hizi za utoaji wa muziki na sababu zinazowafanya wasanii kuzitumia? Katika episode hii, tunafafanua kwa kina maana ya Single, EP, na Album, matumizi yake, pamoja na nafasi yake katika tasnia ya muziki. Kama umewahi kusikia maneno haya lakini hukuwahi kuelewa tofauti zake, basi sikiliza episode h
Episode 98 | "Jizime Data Uende Mjini"
Episode 98 | "Jizime Data Uende Mjini" Jun 29, 2026 913 Episode hii inaangazia umuhimu wa kuwa na aibu yenye afya, huku ikihoji: nini kinaweza kuwa mustakabali wa jamii yetu ikiwa sote tutaendelea kuishi kwa falsafa ya “Jizime data uende mjini”?
Episode 96 | Kwanini Tunahusisha Mateso na Mafanikio?
Episode 96 | Kwanini Tunahusisha Mateso na Mafanikio? Jun 15, 2026 846 Episode hii inaangazia falsafa ya muda mrefu inayodai kuwa mateso na changamoto humjenga mtu kuwa bora, imara, na mwenye uwezo mkubwa wa kufikia mafanikio. Katika mjadala huu, host anachambua na kuunga mkono baadhi ya hoja zinazotolewa na falsafa hiyo, huku pia akitoa tahadhari kuhusu namna inavyoweza kutafsiriwa au kutumiwa vibaya, hasa pale mateso yanapohalalishwa au kuonekana kuwa sharti la maf
Episode 95 | Kwanini Sauti Yako Iliyorekodiwa Husikika Tofauti?
Episode 95 | Kwanini Sauti Yako Iliyorekodiwa Husikika Tofauti? Jun 8, 2026 659 Watu wengi hawapendi kusikia sauti zao zilizorekodiwa na hivyo huamini kuwa wana sauti mbaya. Katika episode hii, tunafafanua kwanini sauti yako iliyorekodiwa husikika tofauti na unavyoijua wewe mwenyewe, na tunajadili hatua unazoweza kuchukua ili kuizoea na kuondoa hisia hiyo.

Recommended