
Nukta the Podcast
Podcast ya Nukta Habari inajadili mada mbalimbali za kijamii, ikiwemo burudani, mitindo ya maisha, safari, teknolojia na biashara. Inalenga kuwafikia wasikilizaji kwa habari na makala zinazogusa maisha ya kila siku. Kila kipindi huchunguza mambo mtambuka yanayowaathiri watu katika jamii ya leo.
Episodes

Hizi ndizo Passport 5 zenye nguvu zaidi duniani
Umewahi kujikuta unatumia muda mrefu katika ofisi ya balozi ya nchi fulani ili kupata viza ?Basi fahamu kuwa baadhi ya watu duniani, usumbufu huo wanausikia TikTok. Pasipoti zao zinatosha kuingia katika nchi mbalimbali. Pasipoti ni hati ya kusafiria ambayo humwezesha raia wa taifa moja kuingia taifa lingine kwa shughuli mbalimbali ikiwemo kazi, biashara, utalii au hata kula bata tu.Licha ya kumili

FIFA kuuza kipande cha nyasi uwanja wa fainali za kombe la dunia kwa Sh1 milioni
Mbio za fainali za Kombe la Dunia zinaendelea kuchanja mbuga huku mashabiki wa nyota wa soka Lionel Messi wakiendelea kutembea kifua mbele mara baada ya timu wa taifa ya Argentina kufanikiwa kumng’oa mwingereza kwa bao moja kwa mbili kwenye hatua ya nusu fainali.Hata hivyo kivumbi na jasho kinatarajiwa kuonekana siku ya Jumapili Julai 19, 2026 ambapo kidume wa mashindano haya makubwa zaidi ya mich

Mambo ya kuzingatia kabla kuwasha gari asubuhi
Je! Unafahamu kuwa asilimia kubwa ya watu wanaoharibikiwa magari yao na kutumia gharama kubwa kufanya matengenezo hutokana na kupuuzia dalili za tatizo husika au kutofanya uchunguzi wa gari yake mara kwa mara?Huenda nawe ni miongoni mwa wasiojua nini wanatakiwa kufanya kabla ya kuwasha gari, oondoa shaka. Kupitia makala haya utaweza kufahamu ni nini hasa unatakiwa kufanya kabla ya kuwasha gari yak

Wanasoka 5 wanaolipwa fedha nyingi zaidi duniani
Wakati macho ya dunia yakielekezwa kwenye fainali za Kombe la Dunia 2026, vita kubwa haipo tu uwanjani katika kusaka ushindi, mabao na taji, bali pia nje ya uwanja ambako nyota wa soka wanaendelea kuvuna mabilioni ya fedha kupitia mishahara, bonasi na mikataba ya matangazo.Kwa mujibu wa jarida la Forbes la nchini Marekani, wachezaji 11 wanaoshiriki Kombe la Dunia la mwaka huu wameingiza kwa pamoja

AHUENI BEI YA MAFUTA KUSHUKA
Huenda watumiaji wa vyombo vya moto nchini Tanzania wakashuhudia ahueni kiduchu mara baada ya bei ya petroli, dizeli na mafuta ya taa kwa mwezi Julai kushuka kulinganisha na ile iliyokuwa ikitumika mwezi Juni.Taarifa ya Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) iliyotolewa usiku wa kuamkia leo Julai Mosi, 2026 inabainisha kuwa bei hizo zimepungua kutokana na kushuka kwa bei ya mafuta katika s

Wizara tano zilizoidhinishiwa fedha nyingi mwaka wa fedha 2026/27
Wakati Bunge la 13 likikaribia kufunga shughuli zake, wizara 27 pamoja na Serikali Kuu zimehitimisha mchakato wa kuwasilisha na kupitisha bajeti zao, hatua inayoweka msingi wa kuanza kwa mwaka mpya wa fedha 2026/27Wizara hizo zilianza rasmi kuwasilisha bajeti zao Aprili 1, mwaka huu na kuhitimisha Juni 2, 2026, ikifuatiwa na Bajeti Kuu ya Serikali iliyoidhinishiwa Sh62.33 trilioni Juni 11,2026 kw

Part 1: Magari 10 yanayotumia mafuta kidogo
Huenda una ndoto ya kumiliki gari kali lenye muonekano wa kifahari, injini kubwa na nguvu barabarani. Pamoja na ndoto hiyo kubwa ila huna uhakika iwapo utaendelea kuwa na kipato cha kulihudumia muda wote. Wasiwasi wako juu kulihudumia gari ni dhahiri kutokana na kuendelea kupanda kwa bei ya mafuta ya petroli hususan miaka ya hivi karibuni. Yafuatayo ni magari 10 yanayotumia kiwango kidogo cha mafu

JINSI MATAPELI WANAVYOPORA MAMILIONI YA WATANZANIA | EP 6
Kila siku baadhi ya Watanzania hutuma fedha kwenda kwa wafanyabiashara wanaotangaza biashara kwenye mitandao ya kijamii kwa matumaini ya kuletewa bidhaa walizochagua.Hata hivyo, baadhi ya wauzaji hao ambao huweka picha zenye mvuto, punguzo kubwa la bei na wenye maelfu ya wafuasi, hupotea bila kuwasilisha hata bidhaa moja.Nyuma ya miamala hiyo kuna uchumi wa utapeli mtandaoni unaotumia ongezeko la

JINSI MATAPELI WANAVYOPORA MAMILIONI YA WATANZANIA | EP 5
Kila siku baadhi ya Watanzania hutuma fedha kwenda kwa wafanyabiashara wanaotangaza biashara kwenye mitandao ya kijamii kwa matumaini ya kuletewa bidhaa walizochagua.Hata hivyo, baadhi ya wauzaji hao ambao huweka picha zenye mvuto, punguzo kubwa la bei na wenye maelfu ya wafuasi, hupotea bila kuwasilisha hata bidhaa moja.Nyuma ya miamala hiyo kuna uchumi wa utapeli mtandaoni unaotumia ongezeko la

JINSI MATAPELI WANAVYOPORA MAMILIONI YA WATANZANIA |EP 4
Kila siku baadhi ya Watanzania hutuma fedha kwenda kwa wafanyabiashara wanaotangaza biashara kwenye mitandao ya kijamii kwa matumaini ya kuletewa bidhaa walizochagua.Hata hivyo, baadhi ya wauzaji hao ambao huweka picha zenye mvuto, punguzo kubwa la bei na wenye maelfu ya wafuasi, hupotea bila kuwasilisha hata bidhaa moja.Nyuma ya miamala hiyo kuna uchumi wa utapeli mtandaoni unaotumia ongezeko la

JINSI MATAPELI WANAVYOPORA MAMILIONI YA WATANZANIA |EP 3
Kila siku baadhi ya Watanzania hutuma fedha kwenda kwa wafanyabiashara wanaotangaza biashara kwenye mitandao ya kijamii kwa matumaini ya kuletewa bidhaa walizochagua.Hata hivyo, baadhi ya wauzaji hao ambao huweka picha zenye mvuto, punguzo kubwa la bei na wenye maelfu ya wafuasi, hupotea bila kuwasilisha hata bidhaa moja.Nyuma ya miamala hiyo kuna uchumi wa utapeli mtandaoni unaotumia ongezeko la

JINSI MATAPELI WANAVYOPORA MAMILIONI YA WATANZANIA | EP 2
SEHEMU YA 2| EPSODE 2. Kila siku baadhi ya Watanzania hutuma fedha kwenda kwa wafanyabiashara wanaotangaza biashara kwenye mitandao ya kijamii kwa matumaini ya kuletewa bidhaa walizochagua.Hata hivyo, baadhi ya wauzaji hao ambao huweka picha zenye mvuto, punguzo kubwa la bei na wenye maelfu ya wafuasi, hupotea bila kuwasilisha hata bidhaa moja.Nyuma ya miamala hiyo kuna uchumi wa utapeli mtandaoni

JINSI MATAPELI WANAVYOPORA MAMIMILIONI YA WATANZANIA MTANDAONI | EP 1
SEHEMU YA 1 | EPSODE 1. Kila siku baadhi ya Watanzania hutuma fedha kwenda kwa wafanyabiashara wanaotangaza biashara kwenye mitandao ya kijamii kwa matumaini ya kuletewa bidhaa walizochagua.Hata hivyo, baadhi ya wauzaji hao ambao huweka picha zenye mvuto, punguzo kubwa la bei na wenye maelfu ya wafuasi, hupotea bila kuwasilisha hata bidhaa moja.Nyuma ya miamala hiyo kuna uchumi wa utapeli mtandaon

AI: jinamizi lingine elimu ya juu Tanzania?
Katika episode hii ya Nukta the Podcast, tunajadili kwa kina namna teknolojia ya akili bandia (Artificial Intelligence – AI) inavyozidi kutumika katika vyuo vikuu nchini Tanzania na mjadala unaoibuka kuhusu athari zake kwa elimu ya juu.Kupitia mahojiano na wahadhiri, wanafunzi, wataalamu wa saikolojia na teknolojia, mjadala huu unaangazia pande zote mbili za AI kama nyenzo ya kurahisisha ujifunzaj

VITA YA MAJI ILIVYOLETA UMOJA KATI YA WAFUGAJI NA WAKULIMA MOROGORO
Katika episode hii tutaangazia jinsi tatizo la maji Ilivyowaunganisha wakulima na wafugaji Kilosa. Hapa utasikia simulizi ya wafugaji na wakulima waliokuwa maadui kutokana na mgogoro wa maji walivyogeuka marafiki baada ya kumfahamu adui wao wa kweli.Kama nilivyoeleza katika episode ya kwanza mimi na producer wangu tulipata wasaa wa kuzunguka baadhi ya vijiji vya wilaya za Kilombero, Kilosa na Moro

HATARI INAYOUKABILI MTO NGERENGERE
Hujambo msikilizaji wa Nukta the Podcast, karibu katika mfululizo wa episode zetu maalumu zinazoangazia Usimamizi wa rasilimali maji pamoja na mazingira katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania. Katika sehemu hii tutamulika hatari inayoukabili Mto Ngerengere uliopo mkoani Morogoro kutokana na uchafuzi unaofanywa wa mto huo. Pia tutachambua hatua zilizochukuliwa na zinazotakiwa kuchukuliwa ili kuun

Wafahamu watu 10 tajiri zaidi duniani 2025
Ukuaji wa teknolojia umeendelea kuchochea ongezeko la utajiri duniani jambo ambalo limesababisha watu waliowekeza katika sekta hiyo kuendelea kujikusanyia ukwasi na kutawala orodha ya watu wenye ukwasi mwingi zaidi duniani.Orodha ya watu matajiri duniani ya mwaka 2025 inayotolewa na Jarida la Forbes la nchini Marekani inaonesha chanzo cha utajiri wa watu 10 matajiri zaidi ni uwekezaji katika tekno

VITA YA MAJI ILIVYOLETA AMANI NA MSHIKAMANO KATI YA WAFUGAJI NA WAKULIMA KILOSA
Katika episode hii tutaangazia jinsi tatizo la maji Ilivyowaunganisha wakulima na wafugaji Kilosa.
Hapa utasikia simulizi ya wafugaji na wakulima waliokuwa maadui kutokana na mgogoro wa maji walivyogeuka marafiki baada ya kumfahamu adui wao wa kweli.
Karibu twende nami mpaka mwisho wa episode hii.

SCRAMBLE FOR WATER RESOURCES
This is the part of the three episodes that we have produced after visiting several districts in Morogoro region, eastern Tanzania meeting with farmers, livestock keepers, environmentalists, factory owners and government officials.
In this first episode we will hear about how pastoralists fight for water resources in Eastern Tanzania due to the increase in demand of water amid ongoing decline of

Restoration of Lake Manyara Tilapia remains an uphill duty
Join Daniel Samson to explore in detail about endangered Manyara Tilapia in Lake Manyara.
Stocks of Manyara tilapias have plummeted to alarmingly low levels in recent decades due to unsustainable fishing.
The International Union for Conservation of Nature (IUCN) Red List of Threatened Species Report 2006 shows that the area of occurrence of the fish, which previously accounted for 73.6% of the t

From sunlight to harvest: How solar energy brings hopes to farmers in Iringa
For decades, farmers in Lupembe Lwa Senga village in Iringa region had relied on the traditional farming system for their livelihoods. Apart from using hand hoes, animal plows, they would wait for the rain to irrigate their crops.
For small plots like gardens, they would use buckets or recently fuel-powered water pumps for irrigation.
“We started irrigation farming as a group in1999, by that

UPUNGUFU WA WALIMU SHULE YA MSINGI UNAVYOATHIRI ELIMU TANZANIA
Wakati watahiniwa zaidi ya milioni moja wa elimu ya msingi Tanzania Bara wakiwa wanasubiri hatma yao, baada ya kumaliza mitihani yao jana Septemba 14, 2023, utoshelevu wa walimu katika ngazi hiyo muhimu ya elimu kwa shule za Serikali umeendelea kuwa kitendawili
Kitabu cha hali ya uchumi cha mwaka 2022, kinabainisha kuwa mpaka Disemba mwaka 2022 kulikuwa na jumla ya wanafunzi milioni 10.8 katika

Elimu ya Veta inavyowainua walemavu wa akili Tanzania
Awali, ilikuwa ni vigumu kushuhudia watu wanaozaliwa na ulemavu wakipata huduma muhimu wanazozihitaji kama elimu, afya, pamoja na kushirikiana na wanajamii wengine kuibua suluhu za matatizo yanayozikabili jamii zao.
Hivi sasa zama hizo zimepita. Kutokana na hatua zilizochukuliwa na Serikali pamoja na wadau, ikiwemo kuielimisha jamii kutowabagua na kushirikiana na kundi hilo, kama binadamu wengin

MFAHAMU MBUNIFU WA MAJIKO YANAYOTUMIA MAWE TANZANIA
Nishati ya kupikia ni miongoni mwa mahitaji muhimu ya binadamu duniani kote, hiyo ndio huwezesha mapishi ya aina mbalimbali za vyakula tunavyokula ili kuimarisha afya na kuwezesha utendaji wa shughuli za kila siku.
Watu wengi wanatambua gesi, mkaa, umeme, mafuta pamoja na kuni kama ndio vyanzo vya nishati ya kupikia kwa kuwa ndio ambavyo vinatumika kwa kiasi kikubwa kwa sasa huku jitihada nyingi z

JINSI MATAPELI WANAVYOTUMIA TAASISI YA MO FOUNDATION KUIBIA WATU
Kama wewe ni mtumiaji wa mtandao wa Facebook huenda umewahi kukutana na chapisho linalohusu fursa ya mikopo kutoka kwenye taasisi ya mfanyabiashara bilionea nchini Tanzania Mohamed Dewji Foundation
Sehemu ya chapisho hilo lianasomeka ‘𝐉𝐈𝐏𝐀𝐓𝐈𝐄 𝐌𝐊𝐎𝐏𝐎 𝐊𝐔𝐓𝐎𝐊𝐀 𝐌𝐎𝐇𝐀𝐌𝐄𝐃 𝐃𝐄𝐖𝐉𝐈 𝐅𝐎𝐔𝐍𝐃𝐀𝐓𝐈𝐎𝐍 kwa maelekezo ya kupata vigezo na masharti njoo hwatspp kwa no👉🏿 0748923136’.
Chapisho hilo pamoja na kuhamasisha wa

KWA NINI BANGI INALIMWA ZAIDI TANZANIA LICHA YA OPARESHENI KALI ZA DAWA ZA KULEVYA?
Mapema Agosti mwaka huu Serikali ya Tanzania ilitangaza kukamata magunia 131 ya bangi, kilo 120 za mbegu za bangi na kuteketeza jumla ya hekari 489 za mashamba ya bangi mkoani Morogoro, katika moja ya operesheni kubwa za kutokomeza dawa za kulevya iliyowahi kufanyika nchini.
Katika operesheni hiyo Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Aretas Lyimo anasema wakul

Teknolojia ya vifuu vya nazi itakavyo waokoa wachimbaji na madhara ya zebaki
Huenda wachimbaji wadogo wa madini Tanzania wakaepukana na athari za afya pamoja na uchafuzi wa mazingira ikiwa wataasili matumizi ya bidhaa mpya ya kusafishia madini (Activated carbon) inayozalishwa nchini.
Bidhaa hiyo inayotengenezwa kwa kutumia vifuu vya nazi itachochea uzalishaji wa madini na kuongeza mchango wa sekta hiyo kwenye pato la taifa kwa kuwa itapatikana kwa urahisi jambo litakalo

Hizi ndio hifadhi tano kubwa za Taifa, Tanzania
Tanzania ni miongoni mwa mataifa ambayo yamebarikiwa vivutio vingi vya utalii ambavyo sio tu vinapendezesha nchi bali ni chanzo kizuri cha mapato hususani fedha za kigeni ambazo hutumika kwa shughuli za maendeleo.
Tovuti ya runinga ya Tanzania Safari Channel ambayo hutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini, inabainisha kuwa Asilimia 40 ya ardhi ya Tanzania imetengwa kwa ajili ya uhifadhi.
Hi

MVUVI MPAMBANAJI NDANI YA ZIWA VICTORIA
Ziwa Victoria ni moja ya maziwa makuu ya Afrika Mashariki. Ni ziwa ambalo lipo kwenye mstari wa ikweta na limezungukwa na nchi tatu zilizopo Afrika Mashariki yaani Tanzania, Kenya na Uganda.
Ziwa hili ni chanzo cha Mto Nile wenye urefu wa kilomita 6,650 na urefu huo unaufanya kuwa mto mrefu zaidi duniani, Ziwa Victoria ndiyo ziwa kubwa zaidi barani Afrika na lina ukubwa wa kilomita za mraba 68,8

ELIMU YA SAIKOLOJIA INAVYOWABEBA WATU WENYE UALBINO TANZANIA
Watu wenye ulemavu wa ngozi nchini Tanzania wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali unyanyapaa ikiwa miongoni, licha ya afua zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali kuelimisha watu wanaowazunguka, baadhi ya walemavu hushindwa kujumuika na wanajamii wengine kutokana na hofu au mitizamo ya kifikra waliyonayo wao wenyewe hata kama jamii ina mtizamo chanya juu yao.
Abdushakur Mrisho ametuandalia

Ifahamu zahanati iliyoanzishwa kwa mkopo wa halmashauri
Ni Zahanati ya Afya ya Jamii iliyopo Kata ya Kipunguni jijini Dar es Salaam ambayo ni ya kwanza katika kata hiyo. Vijana nane wametumia mkopo Sh100 milioni wa Halmashauri ya Ilala kuianzisha ili kupunguza changamoto za afya jijini humo. Esau Ng'umbi anasimulia zaidi.

Mradi wa umemejua unavyowafaidisha wanavijiji Tanzania
Ni mradi wa jiko linalotumia mionzi ya umemejua kupikia vyakula mbalimbali. jiko hilo la aina yake limebuniwa na Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam ili kupunguza matumizi ya kuni na mkaa.

Wazazi wanavyopambana kuwapatia chakula wanafunzi shuleni Pangani
Salaaam msikilizaji wa NUKTA THE PODCAST karibu katika muendelezo wa makala zetu na leo tunasafiri hadi Wilayani pangani mkoani Tanga kumulika namna wazazi wanavyopambana kuwapatia chakula wanafunzi katika shule za sekondari, i mimi ni Suleman Omar Mwiru.

Zaidi ya Watanzania 500,000 kukumbukwa na uhaba wa chakula
Wakati baadhi ya Watanzania wakila na kusaza kiasi cha kutupa chakula, ripoti mpya ya usalama wa chakula na lishe Tanzania inakadiria kuwa kuanzia Mei 2022 watu 592,000 watakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula kutokana na kushuka kwa uzalishaji wa mazao ya chakula katika baadhi ya maeneo nchini.
Ripoti hiyo ya Tathmini ya Usalama wa Chakula na Lishe iliyotolewa Februari 2022 na Wizara ya Kilimo na

“Show” ya kibabe iliyowakutanisha mastaa wa Afrika
‘Young, Famous & African’ au kwa kifupi unaweza kuita YFA, ni ‘reality show’ yaani imebeba uhalisia wa maisha ya wahusika.
Natumaini katika pita pita zako kwenye mitandao ya kijamii, umeshakutana na jina hilo.
Wahusika wake ni vijana nyota, maarufu na wenye ‘mishiko’ yao haswaa kutoka nchi mbalimbali Afrika.
Ndani humo utakutana na ‘Dj’ maarufu kusini mwa Afrika, hapa namzungumzia Dj Naked, mu

Jukumu la kutunza mazingira ni la kila mtu
Utunzaji wa mazingira yanayotuzunguka ni njia mojawapo ya kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi ikiwemo mafuriko na ongezeko la joto.

Ukame ulivyowarudisha wafugaji kwenye umaskini Tanzania
Mwaka 2021 unavyoanza alikuwa ana matumaini lukuki kuwa ng’ombe wake aliokuwa nao wangechangia kwa kiwango kikubwa kumuongezea kipato na kumtoa katika umaskini.
Miezi 11 baadaye ndoto ya Ndirana Ndirana Jijungu, mkazi wa Kijiji cha Mwamihanza wilayani Maswa mkoani Simiyu ilizimwa ghafla kwa kupoteza ng’ombe wanne kati ya sita baada ya kukosa malisho kutokana na ukame. Hata hivyo, ukame wa mwishoni

Mbinu zitakazosaidia kudhibiti taka za baharini
Kudhibiti uchafuzi wa bahari Serikali na wadau wanasema taasisi za utafiti na viwanda zinahitaji kufanya kazi kwa ushirikiano ikiwemo kuimarisha mifumo ya ulejerezaji taka. Pia kupiga marufuku kabisa matumizi ya chupa za plastiki na kutoa elimu kwa wananchi juu ya uhifadhi wa mazingira ya bahari kama anavyoripoti Suleman Mwiru.

Gharama kubwa zinavyorudisha nyuma jitihada za kuokoa mazingira Wilaya ya Kibaha
Baada ya kubaini faida na urahisi wa kutumia nishati ya gesi kupikia, mwalimu wa moja ya shule za sekondari wilayani Kibaha aliamua kuchukua hatua.
Alianza jitihada za kutumia gesi kuongeza ufanisi katika mapishi shuleni kwao na kupunguza kiasi cha kuni zinazotumika kupikia ili kuokoa mazingira. Hata hivyo, changamoto iliyobaki ni gharama kubwa za kupata nishati hiyo. Herimina Mkude anatujuza zaid

Changamoto zinapokuletea fursa
Ni filamu ya "Fine Wine", inayomuhusu mwanadada Kaima anayepitia changamoto katika mahusiano. Licha ya uzuri na ‘usmati’ alionao binti huyu, mahusiano yake na kijana Tunji ni pasua kichwa kuliko hata majukumu yake ya kazi.
Maisha ya Kaima yanabadilika siku ambayo wanakubaliana kukutana na Tunji katika mgahawa fulani, lakini kaka huyo anamwambia mpenziwe kuwa amsubiri kwani kuna jambo la ghafla lim

Taka za kielektroniki zinavyotafuna mazingira ya Tanzania
Hakuna mifumo mizuri ya kutupa taka za kielektroniki nchini Tanzania kama ilivyo kwenye nchi zilizoendelea hivyo suluhu kubwa iliyopo ni kuzitupa kama taka nyingine.

The Last Royal Treasure: Filamu ya kuchangamsha wikiendi yako
Filamu ya ‘The Last Royal Treasure’, inahusu kundi moja la maharamia au kwa Kiingereza wanafahamika kama pirates.
Meli yao imebeba watu ambao wana historia tofauti za kimaisha. Wengine walikuwa majenerali wa vita, watoto wa manahodha, huku wengine wakiwa ni wezi walioshindikana.

Changamoto zinazorudisha nyuma urejelezaji taka Tanzania
Ukosefu wa elimu ya udhibiti wa taka hasa plastiki, sera na sheria zinazosimamia mazingira zimetajwa na wadau wa mazingira kuwa zinaweza zikachelewesha safari ya kupunguza uharibifu wa mazingira hasa unaosababishwa na taka za plastiki.

Chupa za plastiki za vinywaji vya kuongeza nguvu zinavyochocheo uharibifu wa mazingira
Kuzagaa kwa chupa za plastiki za rangi zinazotumika kuhifadhia vinywaji vya kuongeza nguvu katika mitaa mbalimbali nchini Tanzania hasa jijini Dar es Salaam kumeibua changamoto mpya ya kudhibiti uchafuzi wa mazingira.
Licha ya chupa za maji kuokotwa kwa ajili ya kufanyiwa urejelezaji, chupa za rangi zimekuwa zikiachwa zikizagaa mitaani kwa sababu wenye viwanda hawazihitaji katika shughuli zao.&nbs

Magugu maji yanavyowatesa watumiaji wa Ziwa Victoria
Kuendelea kuwepo kwa magugu maji katika Ziwa Victoria kumeibua kadhia mbalimbali kwa watumiaji wa ziwa hilo wakiwemo wavuvi na wamiliki wa boti na meli kwa sababu hutanda katika eneo kubwa na kuzuia shughuli zao.
Wanafanya nini kukabiliana nayo? Msikilize mtangazaji Herimina Mkude ambaye anatoa ufafanuzi zaidi.

Simulizi ya Mtaa unaomezwa na maji ya Ziwa Victoria
Ni Mtaa wa Ziwa mkoani Mwanza ambao umeharibiwa huku nyumba za wakazi wake zikizama kwenye maji baada ya kina cha maji cha Ziwa Victoria.
Kuongeza kwa kina cha maji cha ziwa hilo ni matokeo ya uchafuzi wa mazingira, mafuriko na mvua kubwa iliyonyesha mwaka 2020. Wadau wa mazingira washauri watu kuondoka katika mtaa huo huku wakihimiza watu kuacha kujenga au kufanya shughuli za kilimo na uzal

Mashaka ya maumbile yanavyozuia penzi la kweli
Kwa maringo na mikogo ya Roxanne, unaweza kuhisi ni wa kishua au ana kila kitu lakini huwezi amini, na urembo wake wote alionao, anadaiwa kodi ya pango na kila siku anakimbizana na mwenye nyumba.

Filamu ya Brazen: Maandishi yanayomuwinda mwandishi wa vitabu
Filamu ya “Brazen” inamuhusu mwanamama Grace Miller ambaye ni nyota maarufu wa vitabu vya simulizi nchini Marekani ambaye maandishi yake yanaanza kugeuka uhaisiana kumuwinda.

Kifahamu kisa cha kuumiza kinachoihusu kampuni ya Gucci
Patrizia anavutiwa na kijana mmoja anaekutana naye kwenye party hiyo.
Unaweza kuelezea hisia alizo nazo kama mtu kupata msamaha wa deni la timiza au kuwa zamu katika kupokea hela ya kikoba. Bila shaka unajua hisia hizo.

Filamu: Dunia inampatia mwanamfalme nafasi ya kuchagua kati ya nchi yake na huba.
Izzy anajikuta akivunja kibubu chake alichojitunzia kwa muda mrefu kwa ajili ya kusafiri sehemu mbalimbali duniani.

Utafanya nini pale ndoto yako inapokuingiza matatani?
Siku moja Bom akiwa katika shughuli za kikazi, anaona wafanyakazi wenzie wawili wanapigana, lakini anaposogea kwa karibu anakutana na kitu tofauti.
Mfanyakazi mmoja ametapakaa damu usoni na anapomtazama kwa karibu anagundua kuwa mtu huyo amebadilika na kuwa kama ‘Zombie’.

Ifahamu filamu ‘inayotrend’ kwenye mitandao ya Kijamii Tanzania
Changamoto za mahusiano, malezi, umaskini na mategemeo zote zimeelezewa kupitia wahusika wanne: Tumaini, Angel, Stella pamoja na Rose.

Safari ya ndugu waliopotezana kutafuta ukweli wa wazazi wao
Filamu hii inawahusu mabinti watano ambao kwa mara ya kwanza wanakutana katika moja ya hoteli iliyopo Cancun mjini Mexico.

Kumpoteza mtu umpendaye ni mwanzo wa safari mpya
Filamu hii inamleta tena Buster Moon, mdau wa sanaa za maonyesho ambaye kutengeneza show ya muziki inayoweza kukusanya sayari zote ni kitu kidogo sana.

A Naija christmas : Filamu ya kuchangamsha siku kuu yako.
Filamu hii inahusu familia ya Madam Agatha, singo mother mwenye vijana wa kiume watatu Chike, Obi, na Ugo.

Filamu ya king’s affection: Majukumu yanavyobadilisha jinsia
Filamu hii inaturudisha nyuma enzi hizo wakati nchi ya Joeson haijaitwa Korea. Katika kipindi hicho, Mwana mfalme mteule au “crown prince” Anatarajia mtoto ambaye atakuja kurithi kiti cha enzi kama mfalme wa Joeson.

Itakuwaje ikiwepo sayari ya wanaume peke yao?
Ni filamu inayomhusu mwanadada ambaye anajikuta katika sayari iliyo na wanaume tu baada ya kupata ajali.

Huyu ndiye mwanamke shujaa wa Afrika
Historia ya malkia huyu inatufanya turudi nyuma miaka 500 iliyopita, ambapo Amina akiwa ni ‘princess’ mdogo mwenye ujasiri na kipenzi cha baba yake.

Filamu ya ‘Red Notice’: Kikulacho ki nguoni mwako
Filamu ya “Red Notice”, ipo kutukumbusha kuwa makini na wale wageni wanaogonga kwenye milango ya mioyo yetu na kutufanya tuone kuwa dhamira zao juu yetu ni za dhati.

Filamu ya “No Time To Die”: Mashaka yaliyojaa majuto
Bahati ya mapenzi siyo ya wote, Wakati Adamu akikutana na Hawa kwa urahisi, wengine ni Samson wanaoishia na Delila. Samson wa leo ni James Bond almaarufu kama Agent 007.

Pesa zilivyoweka rehani maisha ya vijana watano
Ni katika filamu ya Filamu ya the Army of Thieves inayohusu kikundi cha wezi waliobobea kuibia mabilionea

“My Name” Filamu ya kuchangamsha wikiendi yako
Katika filamu hii ya “My name”, yaani jina langu, tunakutana na binti mrembo Yoo Ji Woo, ambaye katika maisha yake amekuwa akilelelewa na baba yake tu.
Kwa jinsi baba yake alivyokuwa akimpenda sana, basi Jiwoo anaweza kujiita “dad’s daughter” kama vile wadada huwa wanajigamba.
Maisha ya Jiwoo na baba yake siyo mazuri sana, kwani baba yake hakuwa na kazi rasmi ya kuwaingizia kipato zaidi ya k

Mfahamu ‘single mother’ mpambanaji wa filamu ya Maid
Clean Bandit hawakukosea walipoimba kibao Cha Rockabye, ambacho kinaelezea jinsi single mothers wengi wanavyopambana kwa hali na mali ili kuwalea watoto wao.

Wanawake na safari ya ushiriki maendeleo Kigoma
Ushiriki wa wanawake katika maendeleo ya kata zao umechangia kuwepo kwa huduma muhimu za kijamii ikiwemo shule.

Wema unaosukuma maendeleo ya elimu Tanzania
Kutana na watu wanaochangia maendeleo ya elimu Mkoani Kigoma kwa kuwasaidia wanafunzi kuvuka mto ambao umekuwa kikwazo cha elimu Mkoani humo.

Maisha ya ahueni baada ya Teleza
Teleza ni wahalifu waliokuwa wanajipaka mafuta mwilini au oili na kuwabaka wakina mama mkoani kigoma.

Matumaini mapya baada ya ujenzi wa shule kukwama Kigoma
Endapo serikali itachelewa kukamilisha mradi wa shule hii, huenda ikachangia kwa wananchi kukata tamaa ya kujitoa kwenye shughuli za maendeleo.

Utafanya nini iwapo hakuna anayekuamini tena?
Ni filamu ya “The Last Duel”, inayohusu kufa kwa uaminifu kati ya Marguerite na watu wake wa karibu

Filamu ya The Squid Game: Tamaa mbele mauti nyuma
Uchambuzi wa filamu ya ‘The Squid Game’ inakukutanisha na watu wanaofanya maamuzi magumu baada ya maisha yao kutokuwa na ahueni kila uchao, huku mmoja wapo akiwa ni Gi-Hun.
Hun ni mhusika mkuu katika filamu hii, ambaye maisha yake amekuwa akiyaendesha kwa ‘kuunga unga’ tu, huku kazi yake kubwa ikiwa ni kucheza kamali.

Saa 24 za kummaliza rafiki aliyegeuka kuwa adui
Filamu ya Kate inamhusu mwanadada ambaye hajawahi kufaidi mapenzi ya baba na mama, kwani waliomleta duniani walifariki akiwa bado ni mtoto.

Wananchi wanaopambana kuokoa maisha Geita
Ni kupitia ujenzi wa zahanati ambazo zitatumika kufanya matibabu ya wakazi wa mkoa huo.

Wakazi wa Geita wanavyopambana na kung'oa ujinga
Kutana na juhudi za Wanageita wanavyopambana kung'oa ujinga kwenye mkoa wao

Ushirikishwaji ulivyowainua wanawake Geita
Kutana na Rebecca Makenza, Mwanamke anayehamasisha ushiriki wa wanawake kwenye maendeleo.

Ukatili wa kijinsia sokoni ulivyokomeshwa Dar
Ili kukomesha ukatili wa wanawake kwenye masoko, sheria zimetengenezwa ili kuadhibu yeyote anayefanya udhalilishaji wa kijinsia.

Vita ya baba na mtoto inayoacha alama kwenye familia
Huzuni, hasira na majuto yanamfanya Wenwu kuchochea moto wa kisasi huku kuni yake akiwa ni mtoto wake , Shang Chi.

Hulka ya upole inapobadilika kuwa umafia
Filamu hii ya “The Devil Judge” yaani hakimu shetani inakukutanisha na hakimu ‘mtata’ kuwahi kutokea katika ardhi ya wana filamu.

Zahanati itakayookoa maisha ya maelfu ya wanawake, watoto Geita
Wakazi wa kijiji cha Isebya mkoani Geita wamejenga zahanati itakayopunguza vifo vya watoto na wajawazito wanaosafiri zaidi ya kilomita 5 kufuata huduma za afya kata ya jira ya Ilolungulu.

Kisasi kinavyogeuka kuwa safari ya penzi jipya
Ni filamu ya The Protege, inamhusu mwanadada ambaye waovu wamemaliza familia yake.

Penzi linavyovunja mnyororo wa maisha
Inamhusu mwanababa anayelazimika kubadili maisha yake baada ya mrembo kupita machoni kwake.

The Suicide Squad: Filamu ya waovu wanaobaki tumaini dunia
Pale Superman anapokufa, ulimwengu unabaki bila shujaa wa kumtegemea. Lakini Afisa wa Intelijensia nchini Marekani, Amanda Waller anaishawishi Serikali kuridhia kutengenezwa kwa kikundi cha magaidi walioshindikana.











