Okoka Leo Radio ni kituo cha redio ya kidini (injili) kinachotangaza kwa Kiswahili na Kiingereza. Kazi yake ni kuhabarisha, kukumbusha na kukusisitiza habari ya wokovu wa Yesu Kristo pale msalabani: «Kama hujaokoka basi Okoka Leo, usingoje kesho». Inasikilizwa mtandaoni kupitia Zeno.fm, na ina chaneli ya YouTube 'Okoka Leo Tv' yenye mafundisho ya injili.