Home Podcasts TANAPA PODCAST
TANAPA PODCAST

TANAPA PODCAST

Tanzania National Parks (TANAPA) 16 Episodes Sep 28, 2026

Huu ni podikasti rasmi ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA). Tunachunguza mazungumzo muhimu kuhusu elimu ya uhifadhi, utalii, na fursa za uwekezaji katika Hifadhi za Taifa za Tanzania. Kila kipindi kinaangazia mikakati ya uhifadhi endelevu na ushirikiano muhimu unaosaidia kulinda maliasili zetu kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Episodes

SE02 EP05: Utalii wa Uwajibikaji; Siri ya Uzoefu Bora Kwa Watalii na Uhifadhi Endelevu
SE02 EP05: Utalii wa Uwajibikaji; Siri ya Uzoefu Bora Kwa Watalii na Uhifadhi Endelevu Sep 28, 2026 01:54:29 Sikiliza mwendelezo wa kipindi maalum uweze kufahamu umuhimu wa kufanya utalii wa kiuwajibikaji kwa Waongoza Watalii na dhima yake ya kutunza mazingira, uhifadhi endelevu, kukuza utalii pamoja na kutengeneza uzoefu usiosahaulika kwa watalii wanaotembelea Hifadhi za Taifa.Ni ndani ya TANAPA Podcast – Season 2, Episode 05, ni mazungumzo maalum kutoka kwa Waongoza Watalii wabobezi na Wahifadhi wazoef
SE02 EP04: Utalii wa Uwajibikaji; Siri ya Uzoefu Bora Kwa Watalii na Uhifadhi Endelevu
SE02 EP04: Utalii wa Uwajibikaji; Siri ya Uzoefu Bora Kwa Watalii na Uhifadhi Endelevu Sep 21, 2026 01:31:11 Sikiliza kipindi maalum uweze kufahamu umuhimu wa kufanya utalii wa kiuwajibikaji kwa Waongoza Watalii na dhima yake ya kutunza mazingira, uhifadhi endelevu, kukuza utalii pamoja na kutengeneza uzoefu usiosahaulika kwa watalii wanaotembelea Hifadhi za Taifa.Ni ndani ya TANAPA Podcast – Season 2, Episode 04, katika mazungumzo maalum kutoka kwa Waongoza Watalii wabobezi na Wahifadhi wazoefu.Jumatatu
SE02 EP03: Utalii wa Ndani na Nguvu ya Vyombo vya Habari katika Kutangaza Uzuri wa Serengeti
SE02 EP03: Utalii wa Ndani na Nguvu ya Vyombo vya Habari katika Kutangaza Uzuri wa Serengeti Aug 31, 2026 00:51:39 Nafasi ya vyombo vya habari katika kuhamasisha Watanzania kutembelea vivutio vya utalii.Sikiliza TANAPA Podcast – Season 2, Episode 03 kwa mazungumzo maalum kuhusu utalii wa ndani, nafasi ya vyombo vya habari na namna tunavyoweza kuitangaza Tanzania kwa Watanzania na dunia.Jumatatu, 31.08.2026Eneo: SerengetiMwongoza Kipindi: Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Catherine MbenaNi mwendo wa bandika bandua
S02 EP02 - Ujirani Mwema na Faida Zake kwa Jamii
S02 EP02 - Ujirani Mwema na Faida Zake kwa Jamii Aug 3, 2026 00:48:31 Katika episodi hii utasikia simulizi, uzoefu na ushuhuda kutoka kwa wataalamu wa uhifadhi pamoja na wanufaika wa programu za ujirani mwema, wakieleza namna uhifadhi unavyochangia maendeleo ya wananchi na ustawi wa jamii.Eneo: ArushaMwongoza Kipindi:Afisa Uhifadhi Daraja la Pili, Happiness SamWageni:​ Afisa Uhifadhi Mwandamizi Lameck Matungwa – Kitengo cha Ujirani Mwema, Hifadhi ya Taifa Milima Mah
Promo S02 EP02 - Zifahamu faida za ujirani mwema zitokanazo na uhifadhi kwa jamii
Promo S02 EP02 - Zifahamu faida za ujirani mwema zitokanazo na uhifadhi kwa jamii Jul 28, 2026 00:01:45 Jamii zinazozunguka Hifadhi za Taifa zinanufaikaje na uhifadhi? Sikiliza simulizi na uzoefu wa wadau wa uhifadhi kuhusu namna ujirani mwema unavyochangia maendeleo ya wananchi na uhifadhi endelevu.TANAPA Podcast – Msimu wa 2 | Episodi ya 02Mwongoza kipindi: Happiness Sam (Afisa Uhifadhi Daraja la Pili)Wageni:• Lameck Matungwa – Afisa Uhifadhi Mwandamizi, Kitengo cha Ujirani Mwema, Hifadhi ya Taifa
SO2 EP 01: FAHAMU ELIMU YA UJIRANI MWEMA NA FAIDA ZAKE KATIKA UHIFADHI NA JAMII
SO2 EP 01: FAHAMU ELIMU YA UJIRANI MWEMA NA FAIDA ZAKE KATIKA UHIFADHI NA JAMII Jul 13, 2026 00:45:00 Episodi hii inaangazia - Chimbuko la Elimu ya Ujirani Mwema- Uanzishwaji na malengo yake kwa jamii zinazoishi kuzunguka Hifadhi za Taifa- Faida zake na umuhimu wa ushiriki wa wananchi katika kuhifadhi rasilimali za Taifa kwa kizazi cha sasa na kijachoMgeni Mualikwa: Afisa Uhifadhi Mwandamizi Samwel Nassari, Kitengo cha Uhifadhi – TANAPA Makao Makuu.Host: Afisa Uhifadhi Daraja la Pili Happiness Sam
Promo S02 EP01 Ujio wa Msimu wa II wa Podcast
Promo S02 EP01 Ujio wa Msimu wa II wa Podcast Jul 1, 2026 00:03:38 TANAPA PODCAST | SEASON IITumerejea na msimu mpya wenye simulizi, maarifa na mazungumzo yanayokupeleka karibu zaidi na ulimwengu wa uhifadhi, utalii na uwekezaji katika Hifadhi za Taifa 21 za Tanzania.Tegemea vipindi vilivyoboreshwa, maudhui ya kina, wageni mbalimbali na uzoefu mpya wa kusikiliza.TANAPA PODCAST, HIFADHI ZETU, SAUTI YETU.
S01 EP16 - MILA, DESTURI NA TAMADUNI KATIKA UHIFADHI WA MALIASILI.
S01 EP16 - MILA, DESTURI NA TAMADUNI KATIKA UHIFADHI WA MALIASILI. Nov 24, 2025 00:35:37 Episodi hii inaangazia njia za asili zilizotumika katika utunzaji wa maliasili kwa kufuata taratibu za kitamaduni, mila, desturi na makatazo mbalimbali yaliyosaidia kusimika mizizi imara na kuwa chimbuko la uhifadhi wa kisasa. Hekima za mababu zetu kama vile kuheshimu misitu, kutotumia rasilimali kupita kiasi, na kutambua uhusiano wa binadamu na mazingira vimekuwa dira muhimu inayoongoza mbinu za
S01 EP15 - UHIFADHI NI JUKUMU LA KILA MMOJA
S01 EP15 - UHIFADHI NI JUKUMU LA KILA MMOJA Nov 17, 2025 01:02:33 Episodi hii inakuletea uchambuzi wa kina kuhusu Uhifadhi kwa kuzingatia kuwa Uhifadhi wa wanyamapori ni zoezi la kujitolea kulinda na kuhifadhi maliasili kwa maslahi ya Taifa kwa kizazi hiki ma kijacho.Sikiliza Episodi ya 15 upate elimu kutoka kwa Mzee Ibrahimu Kasontola kutoka katika kijiji cha Lukoma wilayani Uvinza - Kigoma aliyejitolea kwa hali na mali kuhifadhi msitu katika eneo la makazi yak
S01 EP14 - MILA, DESTURI NA TAMADUNI KATIKA UHIFADHI WA MALIASILI.
S01 EP14 - MILA, DESTURI NA TAMADUNI KATIKA UHIFADHI WA MALIASILI. Oct 27, 2025 00:55:20 Episodi hii inaangazia mila, desturi na tamaduni katika uhifadhi wa maliasili, hususan namna jamii ya Wangoni kutoka mkoani Ruvuma ilivyotumia majina na utamaduni wao kulinda Wanyamapori na Misitu  tangu enzi za mababu zetu.Hadithi hii ya kuvutia inaonesha jinsi urithi wa jadi ulivyokuwa chachu ya kulinda rasilimali za Taifa ambazo leo hii zinachangia kwa kiasi kikubwa katika sekta ya uhifadhi na
S01 EP13 - Mila na Tamaduni zilizohusisha mizimu katika kuhifadhi Maliasili
S01 EP13 - Mila na Tamaduni zilizohusisha mizimu katika kuhifadhi Maliasili Oct 20, 2025 00:54:47 Episodi hii inakuletea mazungumzo ya kina kuhusu mila, tamaduni na makatazo ya Kabila la Wagongwe lililopo mkoani Katavi na jinsi taratibu hizo zilivyochangia kulinda maliasili na vyanzo vya maji. Mathalani; ilikuwa hairuhusiwi kukata miti iliyokuwa katika vyanzo vya maji kutokaana na imani ya kuwepo kwa nyoka mkubwa wala kuua mnyamapori hadi upewe kibali na pepo au jini Katabi anayepatikana katik
S01 EP12 - Zoezi la Uhamishaji Tembo kutoka Misenyi kwenda Hifadhi ya Taifa Burigi - Chato.
S01 EP12 - Zoezi la Uhamishaji Tembo kutoka Misenyi kwenda Hifadhi ya Taifa Burigi - Chato. Oct 16, 2025 00:50:02 Episodi hii imeangazia zoezi endelevu la kuwahamisha tembo walowezi kutoka maeneo ya karibu na wananchi kwenda hifadhini na zoezi zima la kuwaswaga tembo waliotoka hifadhini kuvamia maeneo ya wananchi na kuwarudisha hifadhini.Sikiliza Episodi hii kwa taarifa hiyo na mengine mengi kupitia Epsode ya 12.Eneo: Misenyi - Bukoba.Host: Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Catherine MbenaGuests: Kamishna Msaidi

Recommended